ENGLISH FRENCH SWAHILI
Ukurasa
Kuusu sisi
Tunacho fanya
 Mipango yetu
Wazamini wetu
Ripoti za mwaka
Utafiti
Habari
Wasiliana nasi
To top of page


Muungano wa Wanawake wa Fizi kwa Maendeleo ya Jamii - "SOFIBEF"

- ni shirika la wanawake wa vijijini ambalo lina:

  • pigania haki za mwanamke vijijini
  • tetelea afya ya moyoni ya mwanamke aliye hasiliwa na maafa ya vita (vilevile maafa ya nyumbani)
  • tetelea haki ya mtoto.

Hatuko shirika la kizamini.

Sofibef ina fanya kazi zake mnamo mtaa wa Fizi, jimbo la Kivu ya kusini, mashariki ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyo kuwa ina itwa Zaire zamani. Shirika hili lina saidia miradi ya haki na maendeleo ya akina mama toka vijiji vya: Tingi-tingi, Kikonde,, Kazimia, Yungu, Fizi, Mboko, Makobola, Minembwe na Baraka.


KILICHO SABABISHA SOFIBEF IUNDWE

Kila siku katika mtaa wa Fizi, kuna wanawake wanao kabiliwa na matatizo ya uvunjaji wa haki za kibinadamu. Hali hii ime onekana katikati ya mme na mke nyumbani, kati ya mwanamume na mwanamke katika jamaa, katika maisha ya kifamilia kazalika unyanyaso wa wajane, viwete na wazee. Kuna unyanyaso wa kimwili, kinafsi, kiuchumi, kimazingira na kisiasa. Wanawake wengi wanaishi maisha na utamaduni wa kupigwa, kutusiwa, kushitumiwa, kutengwa na kutokushirikishwa katika mazungumzo ya jamaa.

Mtaa una zingatia utamaduni wa mwanamke chini ya mwanaume. Hali hii ya kutofaitisha mwanamke na mwanume ili anza tangia zamani za kale kulingana na asili ya wakaji ambayo ilimtia mume kua kichwa cha muke ambayo ilizingatiwa na dini, serkali na kundi la watu ambao hawapendi mwanamke apate sauti ili atetelee haki zake kwa niaba ya kutia mwanamke awe chini ya miguu ya mwanamume

Rape and other forms of sexual violence were widespread during war. Women were gang-raped, held in sexual slavery, raped with sharp objects, and in other ways sexually mutilated. Women victims were imprisoned in their homes or kept in the headquarters of their torturers as a "feast" for militia men (Mai-Mai), rebels, soldiers, policemen. Some women were forced to follow their rapers into exile as the only means of escaping death. Others were forced to watch as their family members were killed by the rapists, and left to live with the sorrow of absolute loss.

Katika mtaa huu, asili mia 80 ya watoto wasichana wameacha shule kwenye shule za msingi wakijuwa tu kuandika, kusoma na kuhesabia. Inje ya shule ambayo wana acha bado wachanga, watoto wasichana wana tumiwa kwa kazi kali kama vile kulinda wadogo zao wakati mama wako shambani ao mafigani na zaidi sana kwa wale ambao umri ume kua juu, wanafanya kazi kama mama zao. Ndoa imefanyika kwa haraka bila matayarisho yoyote. Hali hii ina leta utata hadi kuishia kwenye kuvunjika kwa ndoa kwa sababu vijana wanaume wanajikuta wana owa mke ambaye elimu ni ndogo hadi kwamba wana amua kwenda mjini ili wajitafutiye wanake walio elimishwa kiasi. Kwa sababu ya elimu ndogo amabyo watoto wanawake wanayo, watoto wao hawana afya nzuri kwa sababu hawajui yanayo pashwa kwa kulinda afya ya watoto vizuri. Kazalika, wajane vile vile wame nyimwa haki zao sababu hawajui vipi kutetelea haki hizo kulingana na elimu hafifu ya kuto kutambua ni ipi haki yao ao ni wapi kwa kwenda ili kufuatilia sheria yao.

Zaidi ya hayo, inastahili kukumbuka kwamba tangia mwanzo wa vita vya ukombozi mnamo jamhuri yetu miaka chache iliyo pita, wanawake wa mkoa wa Fizi walikabiliwa na magumu makali ya kisiasa. Silaa kali na bunduki, zili sambaa popote, nyingi zao zilianguka mikononi mwa rahia na kwa matokeo ya kwamba ili tumiwa kwa kunyanyasa, kutisha, kuuwa na kubaka wanawake. Ubakaji, unyanyaso, kufungwa kwa akina mama ao kutumiwa kama mtumwa wa matumizi ya ndoa na wajeshi ao marahia (mai-mai) ili panda juu sana na kimya kika zunguuka swala hilo. Hakuna aliye jiusisha ili atetelee wanawake katika magumu haya. Wanawake wengi wali achwa katika unyonge na huzuni wa kuona ndugu zao kuuwawa mbele ya macho yao.

Wengi wa wale walio kabiliwa na hali hii ya vita ni wanawake na watoto. Hatari za ubakaji mnamo kipindi hiki ina matokeo mabaya kwa sasa na ita chukuwa mda mwingi hadi wanawake wasahau yalio watokea. Kuna wanawake wengi sasa ambao wali ambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kaswende, gonorea na ukimwi. Wengine wao wali jeruiwa katika sehemu zao za siri kwa sababu ya ujambazi wa wabakaji. Unyonge na uzuni wa kujikuta wana mimba ya watoto ambao hawakuitaji, ili acha akina dada wengi katika hali ya kuji uwa sababu ya kuona kwamba wamepoteza maisha ya kesho. Mbili kwa tatu ya wakaaji wa mtaa wa Fizi ni wanawake, na wengi wa hawa wote wana uzuni moyoni, wajane, na wana garama kubwa ya kulinda watoto wao mayatima.

Sio tu kwamba wanawake wana nyanyaswa kimwili ao kinafsi, hata shirika zao moja moja ziko chini ya utisho wa kufungiwa kazi kwa sababu ya kujitolea kwao kwa mageuzi ya siasa ya udikteta, unyanyaso na utengano.

Utengeno wa umbo uko mwingi mtaani hapa. Fizi ya utamaduni ili mzuiya mwanamke kupata elimu na habari. Hali hii ili ongeza matokeo mabaya ya magonjwa, njaa na kushirikishwa kwa mwanamke mnomo mipangilio ya maendeleo.
Mbele ya hali kama hiyo, mwanamke wa mkoa wa Fizi ali jikuta hana na nafasi ya kwenda ili ajitambue. Ni hapo ndio, wanawake wamoja waliona sio vizuri tuwe tuna ongozwa katika kila jambo. Ni afadhali na sisi tu amuke ili tupaze sauti ya hali hii mbovu ambaya mwanamke wa vijijini alikuemo. Hapo ndio chanzo cha Shirika hili la SOFIBEF.

Kulingana na hali hii ya unyanyaso na ujambazi, SOFIBEF ambaye lengo kubwa ni kuchangia kwa kutambulisha haki ya mwanamke katika mtaa huu, haingeweza kubaki bila kufanya lolote. Mpango ulioko kwa sasa ni kupaza sauti na kusaidia ili mpango wa amani utekelezwe ili haki za mwanamke zitambuliwe na kuheshimiwa. Kuna wanake wengi sasa mtaani hapa ambao, shukrani kwa kampeni za Sofibef wanajuwa ya kwamba wana wajibu wa kuchangiza kuleta amani. Katika kampeni hizo, wanajiusisha zaidi sana na kutetelea uhuru, umoja, usawa na amani. Wanawake wanafanya asili mia 70 ya wakaaji wa mtaa huu. Kwa hesabu hii, wana uwezo wa kuwa ufunguo wa mabadiko mnamo mtaaa. Ila wana itaji msaada wa jumuhia ya kimataifa ili amani na usalama ipatikane mtaanai.